Swahili Language Information from Emergency Management

Weka nyumba na jamaa yako tayari

Majanga huweza kutokea wakati wowote. Ni vema kupanga mapema ili ujishughulikie vilivyo, pamoja na jamaa yako. Kuna hatua tatu ambazo kila mtu anaweza kuchukua zinazoweza kusaidia.       

  • Tayarisha mpango - Jamaa yako huenda isiwe pamoja wakati wa janga kwa hivyo ni muhimu kupanga mapema jinsi ya kuwa mahala salama, jinsi mtakavyowasiliana na mahala pa kukutana baada ya mkasa.     

  • Tayarisha kidubasha - Hakikisha kuna kila kitu kinachohitajika kujisalimisha katika janga. Angalau kuwe na maji, chakula, kurunzi, mavazi ya ziada na blanketi za kuhakikisha joto na kidubasha cha huduma ya kwanza.      

  • Saidiana - Panga na marafiki na majirani ili kusaidiana. Sehemu zifuatazo zitatoa taarifa Zaidi kuhusu jinsi ya kujitayarisha na kutayarisha familia katika majanga.   

TAARIFA ZA KISWAHILI KUTOKA KATIKA USIMAMIZI WA DHARURA